Search
Close this search box.
Africa
Olakira, msanii wa Nigeria

Nyota wa Nigeria na mwimbaji mahiri wa wimbo Maserati, Olakira ameanza mwaka kwa habari njema baada ya kutia saini dili kubwa na kampuni ya magari Maserati.

Habari hizo zilisambazwa kwenye jukwaa la mtandao wa kijamii wa Maserati katika kutambua wimbo “In My Maserati’.

Wimbo huu ulipata umaarufu mkubwa Afrika Mashariki na ulimwenguni kote na kutazamwa na takriban watu milioni 100 kwenye YouTube na majukwaa mengine mtandaoni kote duniani.

Katika video iliyowekwa kwenye ukurasa rasmi wa Instagram, mwimbaji huyo hakuweza kuficha mshangao wake baada ya kupata mkataba huo alipokuwa katika safari nje ya nchi.

Kama sehemu ya mpango huo, nyota huyo atapata fursa ya kutumia magari ya Maserati Luxury Cars katika nchi yoyote atakayotembelea. Mstari ‘Hop in My Maserati’ kutoka kwa wimbo huo umependwa na wanaounda magari hayo.

Hii ni mara ya kwanza kwa watengenezaji wa magari aina ya Maserati kushirikiana na msanii wa Kiafrika.

Comments are closed