Search
Close this search box.
Africa
Mwandishi Kakwenza Rukirabashaija

Mwandishi mashuhuri wa Uganda anayeshutumiwa kwa kuitusi familia ya Rais Yoweri Museveni aliachiliwa Jumatano baada ya kuzuiliwa licha ya amri ya mahakama ya kuachiliwa kwake, wakili wake alisema.

Kakwenza Rukirabashaija, ambaye kesi yake imezua wasiwasi wa kimataifa, alipelekwa na wanajeshi nyumbani kwake mashariki mwa Uganda baada ya kuzuiliwa katika kambi ya polisi ya kijeshi, wakili Eron Kiiza aliiambia AFP.

“Ameachiliwa lakini ni mnyonge sana tumempeleka hospitalini Kampala,” Kiiza aliongeza.

Siku ya Jumanne mahakama iliamuru mwandishi huyo wa riwaya kuachiliwa kwa dhamana,kwa masharti kwamba asizungumze na waandishi wa habari kabla ya kukamilika kwa kesi yake ambapo anatuhumiwa  kumkosea Rais Yoweri Museveni na mwanawe kwenye mitandao ya kijamii.

Lakini wakili wake alisema kuwa badala ya kuachiliwa, mwandishi huyo “alitekwa nyara” kutoka gerezani saa kadhaa baadaye na watu wenye silaha waliovalia nguo za kawaida.

Rukirabashaija — ambaye mawakili wake wanasema aliteswa tangu kukamatwa kwake mwishoni mwa Disemba — alishtakiwa Januari 11 kwa “jumbe za kuudhi” kutokana na msururu wa jumbe zake kwenye Twitter kumhusu Museveni na mwanawe Muhoozi Kainerugaba.

Mwandishi huyo alipata sifa nyingi kwa riwaya yake ya kejeli ya 2020, “The Greedy Barbarian,” ambayo inaelezea ufisadi wa hali ya juu katika nchi ya kubuni.

Alitunukiwa Tuzo ya 2021 ya PEN Pinter kwa Mwandishi wa Kimataifa wa Ujasiri, ambayo hutolewa kila mwaka kwa mwandishi ambaye ameteswa kwa kusema juu ya imani zao.

Amerika, Umoja wa Ulaya na mashirika ya kiraia yalielezea wasiwasi wao kuhusu kuzuiliwa kwake na kutaka aachiliwe.

Comments are closed