Mwigizaji wa Marekani Anne Heche amelazwa hospitalini akiwa katika hali mbaya baada ya ajali ya gari

Mwigizaji Anne Heche alihusika katika ajali baada ya gari alilokuwa akiendesha kugonga nyumba katika kitongoji cha Mar Vista huko Los Angeles siku ya Ijumaa.

Ajali hiyo ilisababisha gari na nyumba kuteketea na dereva kupata majeraha mabaya ya moto.

Kulingana na ripoti ya Polisi wa Los Angeles, dereva huyo alikuwa akisafiri kwa mwendo wa kasi alipotoka barabarani na kugonga nyumba. Mwenye nyumba alikuwa ndani wakati wa tukio, lakini yuko sawa.

Aliigiza katika filamu kadhaa kuanzia miaka ya 1990 zikiwemo “Six Days, Seven Nights,” “Donnie Brasco” na “I Know What You did Last Summer.”

Heche pia anajulikana kwa jukumu lake kwenye filamu ya “Another World” ambayo alishinda tuzo la Daytime Emmy mwaka 1991. Wakati wa miaka ya 1990, alikuwa katika uhusiano wa kimapenzi na mtangazaji wa kipindi cha mazungumzo Ellen DeGeneres.

Chanzo cha ajali hiyo bado kinachunguzwa.