Sehemu ya Nairobi Expressway mnamo Jumatano, Julai 12, alifungwa kwa muda baada ya waandamanaji wanaopinga serikali kuharibu baadhi ya sehemu maeneo ya mlolongo, Kaunti ya machakos.
Hii ni baada ya waandamanaji kubomoa na kuharibu ukuta wa barabara hiyo maeneo hayo na kusababisha uharibifu mkubwa wa mali.
Katika taarifa, mwendeshaji huyo alihakikisha kwamba wanajitahidi kurejesha hali ya kawaida hata kama maandamano dhidi ya kupanda kwa gharama ya maisha yakishika kasi.
Wenye magari katika barabara kuu wameshauriwa kutumia barabara ya JKIA.
Dakika chache mapema, waandamanaji waliharibu kizuizi na vituo vya utozaji ushuru karibu na Mlolongo, Kaunti ya Machakos.
Zaidi ya hayo, usafiri huo ulilemazwa baada ya vijana hao waliokuwa na ghasia kuwasha matairi kando ya barabara ya mwendokasi
Kwenye video zilizoonekana na Radiojambo waandamanji wanaonekana wakiwa na ghadhabu huku wakibomoa sehemu ya barabara ya Express Way Mlolongo kaunti ya Machakos.
Hata hivyo IG Koome alisema kuwa maandamano ambayo yaliitishwa na muungano wa Azimio sio halali.
Hayo yakijiri, Polisi mjini Mombasa wametumia vitoa machozi kuwatawanya waandamanaji wanaoipinga serikali.
Polisi walikuwa wamefunga barabara ya Moi Avenue kuwazuia waandamanaji hao kuingia katikati mwa mji wa Mombasa. Waandamanaji hao wamekuwa wakikabiliana na polisi mitaani kwa takriban saa mbili.
Afisa mkuu wa polisi Mombasa awali alikuwa amewataka waandamaji kutawanyika kwa amani akisema kuwa maandamano hayaruhusiwi popote Mombasa.
“Ndiyo una haki ya kuandamana, lakini hakuna maandamano yanayoruhusiwa popote Mombasa,”Nawaomba mtawanyike na muende nyumbani kwa amani”,,” OCS Bor alisema.
Barabara na biashara zimesitishwa huku maduka yakiwa yamefungwa kwa muda wote wa Jumatano. Polisi waliendelea kushika doria kukabiliana na maandamano kuambatana na agizo la Inspekta Jenerali wa Polisi Japheth Koome aliyeharamisha maandamano ya Azimio.
Viongozi wa Azimio mjini Mombasa wakiongozwa na seneta wa Mombasa Mohammed Faki walikuwa wamearifu kituo kikuu cha polisi kuhusu maandamano yao ya amani yaliyopangwa, lakini wakanyimwa kibali siku ya Jumanne.
Viongozi wengine waliohudhuria ni pamoja na Mbunge wa Kisauni Rashid Bedzimba, mwakilishi wa Kike wa Mombasa Zamzam Mohammed, Mbunge wa Jomvu Badi Twalib na wawkilishi wadi wa Mombasa na makundi ya kutetea haki za kiraia.
Wiki iliyopita, polisi mkoani humo walilazimika kutumia vitoa machozi kuwatawanya waandamanaji.