Jina la kampuni mpya ya utangazaji inayomilikiwa na mcheza tenisi wa Japan Naomi Osaka limezua taharuki nchini Kenya.
Osaka alizindua kampuni mpya ya utangazaji, “Hana Kuma”, kwa ushirikiano na bingwa mara nne wa NBA LeBron James.
Analenga kusimulia hadithi kuhusu vizuizi vya tamaduni tofauti, mwanariadha wa zamani nambari moja duniani alitangaza Jumanne.
“Hana Kuma”, jina la kijapani ambayo tafsiri yake “Flower Bear” ni kampuni itakayotoa hadithi maalum za kitamaduni lakini pia za ulimwengu kwa watazamaji wote” na tayari ina miradi mingi iliyopangwa.
“Kumekuwa na mlipuko wa wabunifu weusi na wa Asia na hatimaye watakuwa na rasilimali na jukwaa kubwa,” Osaka, ambaye ana baba kutoka Haiti na mama Mjapani alisema katika taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu mradi wake mpya zaidi.
“Katika enzi ya mtandao, tunayotayarisha yana mtazamo wa kimataifa zaidi.”
Unaweza kuona hili katika umaarufu wa vipindi vya televisheni kutoka Asia, Ulaya, na Amerika ya Kusini kwamba jambo zuri kutoka eneo moja pia linaweza kupokelewa vyema na ulimwenguni wote.
Kulingana na Forbes, Osaka alikua mwanariadha wa kike anayelipwa pesa nyingi zaidi ulimwenguni kwa mwaka wa 2020 kwa kupata takriban $37m kutokana na orodha ndefu ya mikataba ya udhamini.
Hata hivyo, jina la Hana Kuma limevuma nchini Kenya tangu tangazo hilo lilipochipuka.
Na ingawa jina hilo linasikika kuwa la kuvutia katika lahaja za Kijapani, katika Kiswahili lina maana tofauti kabisa ambayo haipendezi hata kidogo.