Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amethibitisha kuwa atawania kiti cha urais katika uchaguzi wa 2025, ili kuwa mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kuwa rais nchini humo iwapo atashinda. Samia alisema haya katika hafla ya kusheherekea siku ya Kimataifa ya Demokrasia mjini Dar es Salaam.
Rais Samia amesema kuwa rais wakati huu ni kwa kudra ya mwenyezi Mungu na kulingana na sheria za katiba. Rais amewaagiza wanawake kuungana ili kuhakikisha kuwa mwanamke anashinda nafasi hiyo ya urais.
Rais Samia aliingia katika vitabu vya historia baada ya kuapishwa Machi 19 kama rais wa kwanza wa Tanzania kufuatia kifo cha Rais John Pombe Magufuli.