Search
Close this search box.
Africa

Ongezeko la bei ya mafuta nchini Kenya

68

Mamlaka ya udhibiti wa Nishati na Petroli (EPRA) imetangaza bei mpya ya mafuta kwa kipindi cha Septemba 15 hadi Oktoba 14 2021. Katika taarifa ya EPRA ya 14 Septemba lita ya petroli imeongezeka kwa Ksh. 7.58 na itauzwa kwa Ksh.134.72, lita ya dizeli imeongezeka kwa Ksh. 7.94 na itauzwa kwa 115.60 na mafuta ya taa yamepanda kwa Ksh. 12.97 na yatauzwa kwa Ksh. 110.82, bei hizi zikiwa kwa jiji la Nairobi.

Mamlaka ya EPRA imesema bei hiyo inajumuisha 8% ya ushuru,ikiwa ni kulingana na Sheria ya Fedha ya 2018, Sheria ya Mabadiliko ya Ushuru ya 2020 na viwango vya kudhibiti mfumko wa bei kulingana na notisi nambari 194 ya 2020.

Katika mabadiliko ya mwisho, bei ya petroli Nairobi ilikuwa Ksh 127.14 kwa lita, dizeli ilikuwa Ksh. 107.66 na mafuta ya taa ilikuwa Ksh.97.85 kwa lita.

Comments are closed

Related Posts