Pacha wawili kutoka Japan wamethibitishwa na Guiness World Records kuwa pacha wazee zaidi duniani wakiwa na umri wa miaka 107 na siku 300.
Umeno Sumiyama na Koume Kodama wamevunja rekodi iliyokuwa imewekwa na pacha wengine wawili waJapani dada Kin Narita na Gin Kanie walioaga dunia.
Umeno na Koume, walizaliwa 5 Novemba 1913 mjini Shodoshima, Japan.Tangazo la rekodi hiyo mpya lilitolewa Jumatatu 20 Septemba.
Walioshikilia rekodi hiyo awali, pacha Kin na Gin walikuwa na umri wa miaka 107 na siku 175 kabla walipoaga dunia, Kin aliaga dunia Januari mwaka 2000 na Gin akaaga dunia 2001 akiwa na umri wa miaka 108. Kin na Gin walizaliwa 1 Agosti 1892 mjini Nagoya, Japan.Umeno ana watoto wanne na Koume ana watoto watatu.
Umri wa kuishi Japan uko juu zaidi kushinda mataifa mengine duniani na wazee huheshimika sana nchini humo. Mtu mzee zaidi katika rekodi za Guiness,ni Kane Tanaka mwenye umri wa miaka 118.