Pakistan yapitisha adhabu ya kuwahasi wabakaji kwa kutumia kemikali

Sheria mpya Pakistan inatoa adhabu kwa wanaume wenye rekodi ya ubakaji kuhasiwa kwa kutumia kemikali.

Bunge lilipitisha sheria hiyo Jumatano 17 Novemba na ilianza kutumika mara moja, afisa wa serikali Waqar Hussain alisema.

Chini ya sheria mpya ambayo pia inataka wahalifu wa unyanyasaji wa kingono kupewa adhabu kali,Pakistan imeanza kuwahasi kwa kemikali wabakaji kama adhabu inayostahili kwa wabakaji, afisa wa serikali alisema Alhamisi.

Kuhasiwa kwa kemikali, hufanywa nchini Poland, Korea Kusini, Jamhuri ya Czech na baadhi ya majimbo ya Amerika.

Waziri Mkuu Imran Khan alisema kuwa alitaka kuweka adhabu hiyo kutoka mwaka jana baada ya kilio cha kitaifa juu ya kuongezeka kwa visa vya ubakaji. Kisa cha mama aliyetolewa kutoka kwa gari lake akiwa na watoto wake wawili na kisha kubakwa na wanaume wawili kwa mtutu wa bunduki kilizua kilio na ghadhabu ya kimataifa,

kulingana na shirika lisilo la kiserikali la “War Against Rape” chini ya 3% ya wabakaji hutiwa hatiani nchini Pakistan.

Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limetaka uchunguzi ufanyike kuhusu sababu za unyanyasaji wa kingono badala ya kuweka adhabu kali kama hiyo.