Polisi Watia Mbaroni Wanne Kwa Kushiriki Ubakaji Wa Binti

Jeshi la Polisi limetangaza kuwakamata Watuhumiwa Wanne kati ya 6 waliopanga na kutekeleza Ukatili wa Kingono dhidi ya binti aliyeonekana katika Video iliyosambazwa Mitandaoni hivi karibuni

photo courtesy

Kwa mujibu wa taarifa ya Polisi, waliokamatwa ni Clinton H. Damas (Nyundo), Praygod E. Mushi, Amini L. Lema, na Nikson I. Jackson ambao wamepatikana Dodoma na Pwani

Pia, taarifa imeeleza uchunguzi umebaini tukio hilo lilifanyika Mkoani Dodoma Mwezi Mei 2024 na tayari Binti aliyefanyiwa huo amepatikana na amehifadhiwa sehemu salama

Polisi wamekamata watuhumiwa wanne huko Dar es Salaam waliokiuka sheria na kusambaza picha mjongeo wa tukio hilo kwenye mitandao ya kijamii ambao ni Frora Mlombola, Aghatha Mchome, Madatha Jeremiah Budodi na James Nyanda Paulo.

Pia watuhumiwa wanne wamekamatwa kwa tuhuma za kutengeneza na kusambaza taarifa za ongo mitandaoni zinazosema RIP.Binti aliyebakwa na kulawitia akutwa amefariki. Tukio lilifanyika Mei 2024