Raila Atangaza Rasmi Kuanzishwa Kwa Maandamano

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Bwana Raila Odinga ametangaza rasmi kuanzishwa kwa maandamano kuupinga utawala wa Rais William Ruto ambayo ameitaja isiyokuwa serikali halali.

Katika taarifa kali Alhamisi alasiri, Odinga amesema vipengele vya katika ya Kenya inaruhusu maandamano ya amani nchini.

‘’sikiza, Tarehe 20 machi mwaka huu, tunaanza rasmi maandamano ya amani na Litafanyika jijini Nairobi. Maandamano litakuwa la kushinikaza usawa serikalini. Tafadhali makinikeni’’ kasema odinga

‘’Tunawaambia Ruto na Gachagua hatutaendelea kuishi kwa ahadi za uongo’’ kaongeza Odinga

Raila alikuwa ameweka makataa ya siku 14 kwa serikali kushusha bei ya bidhaa muhimu na vile vile kushusha gharama ya maisha. Makataa hiyo ilikamilika tumatano usiku

Kutokana na hayo Raila amesema serikali ya Ruto na Gachagua si halali na kwa hivyo linafaa kufunganya virago na kuondoka afisini mara moja.

‘’Kwa sabau hii, Ruto lazima ajiuzulu’’ akamalizia Odinga