Raila Odinga ashinikiza Tume ya Uchaguzi (IEBC) Kuondolewa

Kiongozi wa Azimio, Raila Odinga

Miezi sita baada ya uchaguzi mkuu kuandaliwa nchini kenya,matokeo ya urais yamezidi kuzua joto la kisiasa,kiongozi wa upinzani na mrengo wake wa Azimio wakisalia kusisitiza hawayatambui matokeo hayo yaliyotangazwa na aliyekuwa mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati katika ukumbi wa Bomas.

“Msimamo wetu unasalia kuwa Rais William Ruto hakushinda uchaguzi wa urais Agosti 9 2022, aliingia Ikulu kwa njia isiyo wazi na kukiuka demokrasia ya wananchi” Raila alidokeza

Odinga sasa anaitaka tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini kenya IEBC kuondolewa na kisha kubuniwa kwa mfumo mpya wa uchaguzi.

“Na tumesema sisi tumependekeza tume ya uchaguzi IEBC kuondolewa,hatutaki tume moja ambayo makao yake makuu yapo Nairobi,Tunataka mfumo mpya wa uchaguzi ambao utajikita katika kaunti zote nchini” Raila Odinga alisema

Mfumo wa uchaguzi marekani ujumuisha kutangazwa kwa matokeo ya mwisho katika majimbo,mshindi akitapatikana kutokana na wingi wa kura alizopata kutoka majimbo.

Odinga amedai kuwa hawatokubali Rais William Ruto kuhusika moja kwa moja katika mchakato wa kuchagua tume ya uchaguzi.

‘Hatutakubali Rais William Ruto na wapambe wake kuteua jopo la kuwachagua makamishna wa tume ya uchaguzi nchini, lazima tuhusishwe kama Azimio kwani sisi ndio wengi” Odinga alisema.

Hata hivyo pendekezo la Odinga limefutiliwa mbali na rais William Ruto ambaye amedai kuwa ni hatua ya kiongozi huyo wa upinzani kutaka kuhitilafiana na uchaguzi wa 2027 kwa faida yake.

“Sisi mambo ya uchaguzi tulimaliza,sasa wale jamaa wanasema hawataki tena uchaguzi uendeshwe na IEBC,mimi nataka kuwaambia wapinzani wangu kuwa IEBC haichagui mtu,ni hawa wananchi wanaamua nani atakuwa Rais”

Kukamilika kwa muhula wa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini kenya IEBC Wafula Chebukati na makamishna Boya Molu na Abdi Guliye mwezi Januari, kulifungua ukurasa mpya wa udhabiti wa nchi, ukurasa ambao haujawahi shuhudiwa awali.

Tume hiyo ya uchaguzi imesalia bila kamishna wakati ambao majukumu makuu yanaanza kujongea kikuu kikiwa kuangazia mipaka ya maeneo tofauti nchini.

Irene Masit ambaye ni kamishna aliyesalia,hana uwezo wa kufanya shughli yoyote kwa tume kwani alisimamishwa kazi kwa muda kutokana na hoja ya kumtimua ofisini, Tume hiyo ikisalia bila nguvu kwani haina idadi ya watu wanaohitajika hili kutekeleza majukumu yake kama ilivyitajwa na mahakama kupitia mswada wa kurekebisha katiba wa BBI.

Licha ya pengo lililoko kuwa wazi, shughuli ya kuwachagua makamishana wapya inaonekana kuendelezwa kwa mwendo wa kobe.

Hata hivyo bado Rais William Ruto hajatangaza nafasi hizo zilizoshikiliwa na aliyekuwa naibu mwenyekiti Juliana Cherera na makamishna Justus Nyang’aya na Francis Wanderi ambao walijiuzulu mwezi disemba 2022 kuwa wazi.

Katika sheria ya awali tume ya huduma kwa bunge (PAC) ilikuwa na nafasi ya kuwateua wanchama wanne katika jopo hilo la uteuzi wa makamishna wa IEBC, chama cha mawakili nchini kilikuwa na nafasi moja huku baraza la kidini nchini likiwa na nafasi.