Rais Samia Awakumbuka Wazee Mwanza Kwenye Sikukuu Ya Eid

Katika kuadhimisha sikukuu ya Eid Al- Fitri na kutamatika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani, Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa mkono wa Eid kwa Kambi ya Wazee Wasiojiweza na Vituo viwili vya watoto yatima Mkoani Mwanza.

Akiwasilisha zawadi hizo katika Kambi ya Wazee Bukumbi- Misungwi, Markazi ya Watoto yatima ya Sharif Said Nyegezi- Nyamagana pamoja na Kituo cha Malezi ya watoto cha Kamanga, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Said Mtanda amesema Rais Samia anaendeleza utamaduni wake wa kuwakumbuka wenye uhitaji hivyo ametoa zawadi ili kusherehekea vyema sikukuu.

Baadhi ya viongozi kutoka kwenye kambi ya kulelea Wazee hao akiwemo Viviani kaiza ambaye ni afisa mfawizi wamemshukuru Mhe. Rais Samia kwa kuwa na moyo wa kutoa na kulikumbuka kundi hilo ambalo nalo linatakiwa kufurahia sikukuu hizi.

Jumla ya fedha zilizotolewa katika Mkoa wa Mwanza ni shilingi milioni 10 ambapo wamenunuliwa jumla ya mbuzi 12, mchele gunia 12, mafuta ndoo kubwa 12, sukari mifuko 12 na soda katoni 90.

Na Mariam John