Rais Teodoro Obiang Nguema Mbasogo, ambaye ameiongoza Equatorial Guinea kwa mkono wa chuma kwa zaidi ya miaka 43, atawania muhula mpya katika uchaguzi wa urais wa Mwezi Novemba, makamu wa rais amesema Ijumaa.
“Kwa sababu ya haiba yake, uongozi wake na uzoefu wake wa kisiasa”, chama tawala kwa kauli moja kilimchagua Obiang kama mgombea wake wa uchaguzi wa Novemba 20, Makamu wa Rais Teodoro Nguema Obiang Mangue — ambaye pia ni mtoto wa Obiang — aliandika kwenye Twitter.
Rais Obiang, mwenye umri wa miaka 80, ndiye kiongozi wa nchi aliyetawala kwa muda mrefu zaidi duniani ukiondoa wafalme.
Chama chake cha Democratic Party of Equatorial Guinea (PDGE) kina viti 99 kati ya 100 katika baraza la chini la bunge linalomaliza muda wake na viti vyote 70 vya seneti.
Lakini haijabainika ni nani atakayetajwa kuwa mgombea wa chama hicho katika kura za urais.
Wakati mmoja, mtoto tajiri wa Obiang Teodoro Nguema Obiang Mangue, aliyepewa jina la utani la “Teodorin”, alionekana kujipanga kugombea katika uchaguzi huo. Hata hivyo, hakuchaguliwa kuwa mgombea mwaka jana.
Chama cha PDGE kilikuwa vuguvugu moja la kisiasa nchini humo hadi mwaka 1991, wakati siasa za vyama vingi zilipoanzishwa.
Lakini Obiang mwenyewe hajawahi kuchaguliwa rasmi kwa chini ya asilimia 93 ya kura.