Notice: Function _load_textdomain_just_in_time was called incorrectly. Translation loading for the wordpress-seo domain was triggered too early. This is usually an indicator for some code in the plugin or theme running too early. Translations should be loaded at the init action or later. Please see Debugging in WordPress for more information. (This message was added in version 6.7.0.) in /home/mwanzotv/public_html/wp-includes/functions.php on line 6114
Rais wa Liberia apunguza mshahara wake kwa 40% - Mwanzo TV

Rais wa Liberia apunguza mshahara wake kwa 40%

Rais wa Liberia Joseph Boakai ametangaza kupunguza mshahara wake kwa asilimia arobaini (40%).
Kwa mujibu wa ripoti kutoka ofisi ya Rais, Boakai ana matumaini ya kuweka mfano wa “utawala unaowajibika” na kuonyesha “mshikamano” na Waliberia.
Hivi karibuni mishahara ya serikali ya Liberia imekuwa ikichunguzwa vikali huku wananchi wake wakilalamikia kupanda kwa gharama ya maisha.
Takriban mtu mmoja kati ya watano anaishi kwa chini ya $2 (£1.70) kwa siku katika jimbo hilo la Afrika Magharibi.
Hatua ya Rais Boakai imepongezwa na watu katika taifa hilo la Afrika Magharibi huku wengine wakionekana kutilia shauku kutokana na kwamba bado anapokea marupurupu kama vile posho ya kila siku na bima ya matibabu.
Bajeti ya ofisi ya rais nchini Liberia ni karibu $3m mwaka huu.
Ikumbukwe kuwa mshahara ya mtangulizi wake Rais Boakai,George Weah, wakati akiwa uongozini ilikatwa kwa asilimia 25.