Rais Wa Marekani Joe Biden amkaribisha Rais William Ruto Ikulu White house

Rais wa Kenya WilliamRuto alifanya mazungumzo na mwenzake wa Marekani Joe Bidden kwenye ikuli ya White House nchini Marekani Jumatano usiku.

Ulikuwa mkutano wa kwanza wa Rais Ruto na Biden katika ziara yake punde baada ya kuwasili kutoka jimbo la Georgia.

Kwenye kikao hicho Marais hao wawili walizungumzia maswala ya teknolojia kwa kirefu,huku Ruto akimshukuru Rais Biden kwa kuwekeza kiwango kikubwa cha pesa katika miradi ya kiteknolojia  nchini Kenya .

Maafisa wakuu wa utawala walisema Biden na Ruto watajadili masuala mbalimbali kutoka biashara hadi msamaha wa madeni na njia ya kusonga mbele kwa ajili ya Haiti, Ukraine, Sudan na maeneo mengine.

“Ninapanga kwenda mwezi Februari baada ya kuchaguliwa tena,” Biden alisema alipokuwa akimsalimia Rais wa Kenya William Ruto alipowasili Ikulu katika siku ya kwanza kati ya mbili za mikutano na chakula cha jioni.

Ruto ambaye yuko Marekani kwa ziara rasmi ya siku nne pia alikutana na Spika wa Bunge la waakilishi Mike Johnson, ambapo pia alijadiliana na Maseneta kadhaa wakiwemo wa chama cha Democrat na Republican.

Rais wa Marekani Joe Biden alisema anapanga kufanya ziara rasmi barani Afrika mwezi Februari baada ya uchaguzi wa rais wa Marekani, tangazo ambalo linabashiri kuwa atamshinda Donald Trump.

Biden, ambaye ni Mdemokrat, anawania muhula mwingine katika uchaguzi wa Novemba 5 dhidi ya mpinzani wake wa chama cha Republican, Rais wa zamani Donald Trump.