Rais mteule wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud alitumia hotuba yake ya kuapishwa siku ya Alhamisi kuomba msaada wa kimataifa ili kukabiliana na njaa inayotishia nchi yake.
Mashirika ya misaada yameonya kuhusu njaa huku visa vya utapiamlo miongoni mwa watoto vikiongezeka katika taifa hilo la Pembe ya Afrika, kufuatia mvua kukosa kunyesha kwa misimu minne.
âKuna hofu kwamba njaa inaweza kutokea katika baadhi ya maeneo,â Mohamud alisema, na kuwataka âwanadiaspora na ulimwengu kuchukua jukumu katika kuokoa watu wetu ambao wameathiriwa na ukame.â
âHali hizi zilisababishwa na mlundikano wa matatizo yakiwemo mabadiliko ya tabianchi, uharibifu wa rasilimali zetu za kiuchumi na udhaifu wa taasisi zetu za Serikali, hivyo Serikali yangu itaanzisha wakala wa masuala ya mazingira,â alisema.
Mohamud ni mwanaharakati wa zamani wa elimu na amani, muhula wa kwanza wa Mohamud ulikumbwa na kashfa kubwa za ufisadi na misukosuko ya kisiasa, na wawili kati ya watatu ya maafisa wa serikali aliowateua kama mawaziri walilazimika kuondoka, na magavana wawili wa benki kuu kujiuzulu
Mohamud ni kiongozi wa kwanza wa Somalia kushinda muhula wa pili wa urais, ameahidi kuigeuza Somalia kuwa ânchi ya amani katika mipaka yake na amani na mataifa mengineâ na kurekebisha uharibifu uliosababishwa na migogoro ya kisiasa ya miezi kadhaa, katika ngazi ya serikali na kati ya mataifa na serikali kuu serikalini.
Siku ya Alhamis aliapa kukuza âutulivu wa kisiasa kupitia mashauriano, kuridhiana, na umoja kati ya…serikali ya shirikisho na nchi wanachama wa shirikisho,â akitoa mwelekeo tofauti na mtangulizi wake Mohamed Abdullahi Mohamed, anayejulikana zaidi kama Farmajo.
Washirika wa kimataifa wa Somalia wamekaribisha kuchaguliwa kwa Mohamud, huku wengi wakitumai uongozi wake utamaliza mgogoro wa kisiasa wa muda mrefu ambao umeivuruga serikali kukabiliana na uasi wa Al-Shabaab na ukame mbaya.
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia ulitoa taarifa kwenye Twitter na kusema âunampongeza Rais Hassan Mohamud kwa kuapishwa leo, na unatarajia kufanya kazi na utawala wake katika kuunga mkono kuafikiwa kwa vipaumbele vya kitaifa.â
Wakati huo huo, wito wa msaada wa kimataifa umechangisha chini ya asilimia 20 ya fedha zinazohitajika kuepusha kurudiwa kwa njaa ya mwaka 2011 nchini Somalia ambayo iliua watu 260,000 — nusu yao wakiwa watoto chini ya umri wa miaka sita.