Rais William Ruto Afafanua Mbona Aliwateuwa Manaibu Waziri 50

Rais William Ruto ameeleza ni kwa nini alikubali watu 50 aliowachagua kwa nyadhifa za mawaziri wasaidizi

Akizungumza Alhamisi wakati wa hafla ya kuapishwa kwao, Ruto alisema uteuzi huo ulifanywa kimakusudi kwa sababu anajua takriban aliyowachagua wamewai kuhudumu katika nyadhifa tofauti hapo awali

Rais alisema kutokana na hilo, anaelewa wengi wao wanafahamu vyema utoaji wa huduma kwa wananchi ni nini, hivyo kuamua kufanya nao kazi.

Aliwahimiza CAS wapya walioapishwa kuleta uzoefu sawa na ambao wamekuwa nao hapo awali katika utumishi wa umma.

“Nimewateua baadhi yenu kwa makusudi kwa sababu nafahamu kuwa mnaelewa zaidi utumishi kwa wananchi kutokana na uzoefu wenu katika kutumikia nyadhifa nyingine na ninatarajia mlete uzoefu mlioupata sehemu nyingine katika utumishi wa wananchi wa Kenya katika majukumu yako mapya,” Ruto alisema.

Ruto aliwakumbusha manaibu mawaziri hao kwamba Wakenya wana matarajio makubwa ya utawala wa Kenya Kwanza na sasa serikali imeundwa vikamilifu na  wanapaswa kutekeleza wajibu wao.

Ruto aliongeza kuwa wananchi wanahaki ya kupata huduma vikamilifu na wamemsadie kutimiza ahadi alizoweka wakati wa kampeni

“Sasa tukiwa na serikali kamili, hakuna sababu hatuna sababu ya kutoweza kutekeleza ajenda kutoka chini ya kiuchumi ambayo utawala wetu ulichaguliwa nayo.”

Wengi waliyo teuliwa na rais ni wanasiasa haswa waliyobwagwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka WA 2022