Hatimaye Rais William Ruto Jumanne Septemba 27 alifichua majina ya wanaume na wanawake ambao amewateua kuketi katika Baraza lake la Mawaziri na kumsaidia katika kuratibu shughuli za idara za serikali anapoanza kutekeleza ahadi zake katika manifesto yake ya kampeni.
Kama inavyotarajiwa na pande nyingi, Baraza la Mawaziri la Rais Ruto liko mbali na lile la mtangulizi wake, rais wa zamani Uhuru Kenyatta.
Uteuzi huo umewapendelea washirika wengi wa karibu wa Rais Ruto wa kisiasa na hata zaidi viongozi wa zamani ambao waliamua kutogombea viti vyovyote vya ubunge katika uchaguzi wa Agosti ili kuelekeza juhudi zao katika kumpigia debe Mkuu wa Jimbo la sasa kitaifa.
Baadhi ya wanasiasa wanaohusishwa na Kenya Kwanza ambao walishindwa kunyakua au kutetea viti vya kuchaguliwa katika kura hiyo pia wametuzwa nyadhifa za baraza la mawaziri na Rais Ruto.
“Leo, ninajivunia kuwatangaza wale ambao watahudumu katika Baraza la Mawaziri la Jamhuri ya Kenya. Ni muhimu kuunda Baraza jipya la Mawaziri mapema ili kuchukua jukumu na kutimiza mipango na ajenda tuliyoahidi kwa watu wa Kenya. “Pia ninashukuru vyama vya kisiasa vilivyojiunga nasi, UDA, kuunda muungano wa Kenya Kwanza. Kutoka Ford-Kenya hadi Maendelo Chap Chap na wengine,” Ruto alisema.
Hii hapa ni orodha ya walioteliwa katika Wizara mbali mbali;
1. Waziri wa Usalama wa Ndani β Prof Kithure Kindiki
2. Waziri wa Masuala ya Kigeni β Dkt Alfred Mutua
3. Waziri wa Elimu β Ezekiel Machogu
4. Waziri wa Kawi β Davis Chirchir
5. Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki β Rebecca Miano
6. Waziri wa Ulinzi β Aden Duale
7. Waziri wa Utalii β Penina Malonza
8. Waziri wa Afya β Susan Nakumicha Wafula
9. Waziri wa Michezo β Ababu Namwamba
10. Waziri wa Ardhi β Zacharia Mwangi Njeru
11. Waziri wa Leba β Florence Bore
12. Waziri wa Biashara β Moses Kuria
13. Waziri wa Maji β Alice Wahome
14. Waziri wa Mazingira β Roselinda Soipan Tuya
15. Waziri wa Fedha β Profesa Njuguna Ndungβu
16. Waziri wa Habari na Mawasiliano β Eliud Owalo
17. Waziri wa Kilimo β Franklin Mithika Linturi
18. Waziri wa Huduma za Umma, Jinsia na Usawazishaji β Aisha Jumwa
19. Waziri wa Barabara β Kipchumba Murkomen
20. Waziri wa Sekta ya Biashara Ndogo na za Wastani (SMEs) β Simon Chelugui
21. Waziri wa Uchimbaji Madini β Salim Mvurya
22. Mshauri wa Shirika la Masuala ya Wanawake β Harriet Chigai
23. Mshauri wa Masuala ya Usalama wa Ndani β Monica Juma
24. Mwanasheria Mkuu β Justin Muturi
25. Katibu katika Baraza la Mawaziri β Mercy Wanjau