Familia ya aliyekuwa Waziri Mkuu nchini Kenya Raila Odinga, imetangaza ratiba ya mazishi, huku mazishi yakipangwa kufanyika siku ya Jumapili katika Shamba la Opoda, Bondo, Kaunti ya Siaya. Maandalizi haya yanakusudia kuheshimu wosia wa Raila aliyeelekeza azikwe ndani ya saa 72 tangu kifo chake, pamoja na kuzingatia taratibu na mipango ya kurudisha mwili kutoka India.
Alhamisi Oktoba 16
- Saa mbili na nusu asubuhi: Mwili kuwasili JKIA kutoka Mumbai, India, kisha kupelekwa Lee Funeral Home.
- Saa sita–Saa kumi na moja mchana: Kuaga kwa umma katika Jengo la Bunge, kisha kurejeshwa Lee Funeral Home / au kesha ya maombolezo nyumbani Karen jioni.
Ijumaa Oktoba 17
- Saa mbili asubuhi: Ibada ya kitaifa ya kuaga katika Uwanja wa Nyayo, Nairobi.
- Jioni: Mwili kupelekwa nyumbani Karen kwa kesha ya usiku.
Jumamosi Oktoba 18
- Asubuhi: Mwili kupelekwa Kisumu.
- Saa 3 asubuhi–saa tisa jioni: Kuaga kwa umma katika Uwanja wa Moi, Kisumu.
- Mchana/Jioni: Msafara kuelekea Bondo kwa kesha ya usiku.
Jumapili Oktoba 19
- Asubuhi: Mazishi katika Shamba la Opoda, yatakayoongozwa na Kanisa la Anglikana.
Kamati ya mazishi inaongozwa kwa pamoja na Naibu Rais Kithure Kindiki na Seneta wa Siaya Oburu Odinga, na inaratibu shughuli zote. Rais William Ruto alitangaza siku saba za maombolezo ya kitaifa, na bendera zipeperushwe nusu mlingoti nchini na katika balozi za Kenya nje ya nchi. Vilevile, maeneo ya umma yameainishwa kote nchini ili wananchi waweze kufuatilia matangazo ya moja kwa moja na kuaga kwa utulivu na heshima.