Ronaldo atangaza kifo cha mwanawe wa kiume

Cristiano Ronaldo na mpenzi wake Georgina Rodriguez walitangaza Aprili 18 kuwa mtoto wao mchanga amefariki dunia. (Photo by OSCAR DEL POZO / AFP)

Cristiano Ronaldo na mpenzi wake Georgina Rodriguez wametangaza Jumatatu kuwa mtoto wao mchanga amefariki dunia.

Ronaldo alifichua katika chapisho la mtandao wa kijamii Oktoba mwaka jana kwamba wanandoa hao walikuwa wanatarajia mapacha.

Katika chapisho lililotolewa kwenye akaunti ya Twitter ya beki huyo wa Manchester United, walithibitisha kuzaliwa kwa mtoto wa kike.

“Ni kwa huzuni kubwa tunalazimika kutangaza kwamba mtoto wetu wa kiume ameaga dunia. Ni maumivu makubwa zaidi ambayo mzazi anaweza kuhisi,” Ronaldo na Rodriguez walisema katika taarifa waliyotia saini kwa pamoja.

“Kuzaliwa kwa mtoto wetu wa kike kunatupa nguvu ya kuishi wakati huu kwa matumaini na furaha. Tungependa kuwashukuru madaktari na wauguzi kwa msaada wao wote wa kitaalam.

“Sote tumesikitishwa na tukio hii na tunaomba faragha katika wakati huu mgumu sana.”

Wanandoa hao waliokutana wakati Ronaldo alipokuwa akichezea Real Madrid, wana mtoto wa kike mwenye umri wa miaka minne pamoja, huku Ronaldo akiwa na watoto wengine watatu.

“Uchungu wako ni uchungu wetu, Cristiano,” Manchester United walitweet.

“Tupo nawe na familia yako kwa wakati huu.”

Real Madrid pia walijibu katika ukurasa wao wa mtandao kwamba klabu, “Rais wake na Bodi ya Wakurugenzi wake wanasikitika sana kutokana na kifo cha mmoja wa watoto ambao mpendwa wetu Cristiano Ronaldo na mpenzi wake, Georgina Rodriguez, walikuwa wanatarajia. Real Madrid inaungana na familia nzima wakati huu wa huzuni.”

Cristiano Ronaldo na mpenzi wake Georgina Rodriguez walitangaza Aprili 18 kuwa mtoto wao mchanga amefariki dunia (Photo by OSCAR DEL POZO / AFP)