Ruto azuru Sudan Kusini kuzindua upya mpango wa amani wa ‘Tumaini’

Rais wa Kenya William Ruto alikuwa katika ziara rasmi mjini Juba nchini Sudan Kusini Jumatano Novemba 6, 2024 kwa lengo la kuwezeshwa kuanzishwa tena kwa mazungumzo ya amani. Mchakato huu sambamba wa amani, unaoitwa Tumainiambao unafanyika chini ya uangalizi wa Kenya, kati ya serikali ya Sudani Kusini na makundi ya upinzani ambayo hayajatia saini makubaliano ya amani ya mwaka 2018, ulianzishwa Mei 2024 na William Ruto kwa ombi la Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir.

Baada ya maendeleo na kutiwa saini kwa itifaki tisa mwezi Julai, Makamu wa Rais Riek Machar alitangaza kujiondoa kwenye majadiliano. Riek Machar anasalia kuwa mpinzani mkuu wa Rais Salva Kiir, ingawa wanafanya kazi pamoja katika serikali ya umoja na ya mpito iliyoundwa chini ya makubaliano ya amani ya mwaka 2018.

Lakini ziara ya William Ruto inaonekana kuruhusu kuanza kwa zuio la kuanza kwa majadiliano nchini Kenya. Taarifa ya pamoja kwa vyombo vya habari imetangaza bila maelezo zaidi kuanza tena kwa mchakato wa upatanishi wa Tumaini “kusuluhisha matatizo yaliyosalia ndani ya wiki mbili”.

Katika picha zilizochapishwa kwenye ukurasa wa mtandao wa X wa William Ruto, anaonekana akitembea bega kwa bega na Rais Salva Kiir na Naibu Rais Riek Machar – kidokezo kinachoonyesha uwezekano wa maelewano kati ya Rais Salva Kiir na naibu wake. Riek Machar alijiondoa katika mchakato wa Tumaini, akihofia kwamba ungechukua nafasi ya makubaliano ya amani ya 2018 na kudhoofisha msimamo wake ndani ya serikali.

Kwa hakika, mpango wa upatanishi wa Tumaini unaonekana, kulingana na vyanzo kadhaa vya kidiplomasia, kama njia inayowezekana ya kutoka katika mkwamo wa sasa wa mchakato wa amani wa Sudan Kusini. Lakini “hata kama Machar atarejea katika mchakato wa Nairobi,” anasema mtafiti Daniel Akech Thiong wa Kundi la Kimataifa la Migogoro, “njia ya kufikia makubaliano mapya ya pamoja haina uhakika.” Chanzo cha mfarakano mkubwa, kulingana na mtaalamu huyu, swali ni “jinsi ya kuoanisha makubaliano ya amani ya mwaka 2018 na mpango wa Nairobi” na kuamua “ni upi unafaa kutawala”