Saudi Arabia yaahirisha kunyongwa kwa raia wa Kenya

Raia wa kenya anayetarajiwa kunyongwa katika taifa la kiarabu, Saudi Arabia amepata afueni ya dakika za mwisho kufuatia kampeni kubwa ya mitandao ya kijamii.

Stephen Munyakho alihukumiwa kifo mwaka wa 2011 kufuatia mapigano makali na mwenzake katika taifa la Ghuba.

Munyakho ni mwana wa mwanahabari mkongwe Dorothy Kweyu

Kulingana na kampeni ya ”Bring Back Stevo”, inayoendeshwa na wafuasi wake, wafanyakazi wote walipata majeraha ya kuchomwa kisu lakini ni Munyakho, pekee ndiye aliyenusurika. baada ya kesi hiyo, alihukumiwa kifo.

Chini ya sheria za Saudia, hukumu ya kifo inaweza kuondolewa ikiwa familia itakubali kulipwa fidia badala yake.

Familia yake ya nyumbani nchini Kenya imekuwa ikijaribu kutafuta pesa zinazohitajika, ambazo ni riyal milioni tatu na nusu za Saudia (dola 940,000), kwa ajili ya familia ya marehemu, ili kumuokoa Munyakho.

Siku ya Jumatatu, siku mbili tu kabla ya Munyakho kunyongwa, Katibu mkuu  wa Masuala ya nje wa Kenya Korir Sing’oei alisema Saudi Arabia imekubal ombi la serikali la kuahirisha kifo hicho ili kuruhusu mazungumzo zaidi kati ya pande zote.

https://twitter.com/SingoeiAKorir/status/1789980968016629797