Bingwa mara nane wa dunia Sebastien Ogier ndiye mshindi wa Safari Rally ya Ubingwa wa Dunia wa WRC mwaka huu. Ogier alikuwa akishirikiana na mwenzake Vincent Landais.
Mwendeshaji kasi huyo wa kutumia gari ainaya Toyota Gazoo alitumia muda wa saa 3:30:42.5 na kuibuka bingwa wa mkondo wa sabini za mbio za kilomita 1191.06, akimshinda mwenzake na bingwa wa dunia, Kalle Rovanpera kwa sekunde 6.7 katika mbio hizo zilizokamilika jana, mjini Naivasha.
Toyota pia iliambulia nafasi za tatu na nne, ambazo zilikwenda kwa Elfin Evans na Takamoto Katsuta, .
Huu ni ushindi wa pili kwa Ogier katika Safari, baada ya kushinda awamu ya 2021 wakati wa kurejea kwa mbio hizo za kimataifa baada ya mapumziko ya miaka 19.
Mara ya kwanza ya Toyota kupata ushindi wa mfululizo wa 1 hadi 4 ilikuwa mwaka wa 1993.
Mkenya Carl flash Tundo alimaliza mbio hizo katika nafasi ya 12 kwa muda wa saa 4:11:38.6.
Thierry Neuville na mwenzake Esapekka Lappi ambao huendesha gari aina ya Hyunai walimaliza wa 8 na 13 mtawalia.
Mbio hizo zilihudhuriwa na rais wa kenya William ruto ambaye aliwapongeza na kisha kuongoza hafla ya kuwatuza washindi.
Baadaye waliyehuduria sherehe hizo za safari Rally ya kupendeza walipata fursa ya burudani ya kipkee iliyoandaliwa na serikali chini ya mradi wa Talanta Hella. Wengi walihudhuria sherehe na kupata fursa ya kutumbuizwa na wasani tajika kama Khaligraph Johns (OG), Mejja, Femi One, Ssaru Miongoni mwa wasani wengine tajika na wa kuibukia. Talanta Hela ni mradi wa serikali ya kutambua vipaji na kuhakikishi vipaji vinalipa