Nahodha wa Senegal Sadio Mane, ambaye alitinga mkwaju wa penalti wa mwisho na kuiwezesha Senegal kushinda fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya Misri, alitangazwa kuwa mchezaji bora wa michuano hiyo mjini Yaounde siku ya Jumapili.
Mkwaju wake ulisawazisha mikwaju ya penalti baada mlinda mlango Mohamed Abou Gabal kupiga kiki kali kwa niaba ya Misri.
Mane, ambaye alimshinda mwenzake wa Liverpool, Mohamed Salah, alikuwa miongoni wachezaji wa timu ya Senegal iliyoshindwa na Algeria katika fainali miaka mitatu iliyopita mjini Cairo.
Kipa wa Senegal Edouard Mendy alichaguliwa kama kipa bora zaidi wa mchuano huo, licha ya umahiri wa Abou Gabal wa Misri katika kinyang’anyiro hicho.
Kando na kuzuia penalti ya Mane katika muda wa kawaida, Abou Gabal aliokoa mikwaju mingi na kuikosesha Senegal bao katika muda wa kawaida na wa ziada wa fainali hiyo, Gabal alilia baada ya kukosa kuzuia mikwaju ya penalti.
Abou Gabal alikuja Cameroon kama chaguo la pili baada ya Mohamed Elshenawy,kujeruhiwa katika mchuano wa hatua ya 16 bora dhidi ya Ivory Coast.
Nahodha wa Cameroon Vincent Aboubakar alipokea tuzo ya ‘Golden Boot’ kwa kuwa mfungaji bora akiwa amefunga mabao nane, yakiwemo mawili katika ushindi dhidi ya Burkina Faso.
Alikosa kufikia rekodi ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika ya mabao tisa iliyowekwa mwaka 1974 na marehemu Ndaye Mulamba wa Zaire (baadaye iliitwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo)