Search
Close this search box.
Africa

Senegal yatangaza maombolezo ya kitaifa baada ya ajali ya basi kuua makumi

12

Rais wa Senegal Macky Sall.

Watu 38 wamepoteza maisha yao hadi kufikia sasa huku wengine 80 wakipata majeraha mabaya baada ya mabasi mawili kugongana ana kwa ana katika eneo la Senegal ya kati asubuhi ya jana jumapili.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ambayo imetolewa na rais wa taifa hilo Macky Sall.

Ajali hiyo ambayo ni moja wapo ya ajali mbaya zaidi katika kumbukumbu ya taifa hiyo la Afrika Magharibi, ilitokea katika moja wapo ya barabara kuu ya mashariki kuelekea Magharibi mwa mji wa Kaffrine, kilomita 220 kaskazini mwa mji mkuu wa Dakar.

Sall amesema kwenye mtandao wake wa twitter kwamba, amehuzunishwa sana na ajali hiyo na kutangaza siku tatu za maombolezo kuanzia leo jumatatu.

Taarifa kutoka kwa usimamizi wa eneo hilo linaarifu kuwa ajali hiyo ilitokea baada ya gurudumu la basi moja la abiria kupasuka na kupigiria hadi kwa basi nyingine ambalo lilikuwa linakuja kupitana nalo.

Kanda za video kutoka eneo la tukio zilizopachikwa mitandaoni, zilionyesha mabasi mawili meupe yakiwa yamegongana uso kwa uso. Uchafu vilevile ulikuwa umetapakaa kwenye barabara nyembamba.

Ajali za barabara zimeongezeka nchini Senegal, ambapo malori makubwa  na mabasi ambayo mara mingi yametumiwa kwa miongo kadhaa yakiwa yamezeeka huharibu barabara zenye njia mbili zilizo na mashimo na kuharibiwa kwa matumizi kupita kiasi.

Mnamo mwaka wa 2017, mabasi mawili yaligongana na kusababisha vifo vya watu 25, wakiwemo wengine waliokuwa wakienda kwenye tamasha la kidini.

Comments are closed

Related Posts