Serikali ya Kenya yaanzisha msako dhidi ya raia wa kigeni nchini.

Serikali imeanzisha msako dhidi ya raia wa kigeni  wa asili ya Asia wanaoaminika kuingia nchini kinyume cha sheria, wengi wa wageni hao wanaaminika kutokea Pakistan.

Asubuhi ya Alhamis Septemba 30, maafisa wa polisi wakishirikiana na wale wa uhamiaji walifika katika mitaa tofauti jijini Nairobi kuthibitisha iwapo wageni hao waliingia nchini kihalali.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na wizara ya Mambo ya Ndani, raia wa kigeni 20,000 wameinga nchini tangu mwezi Juni.

Katibu Mkuu wa Mambo ya Ndani, Karanja Kibicho amewaamuru maafisa wa uhamiaji kuthibitisha jinsi wageni hao walivyoingia nchini,operesheni hiyo imeanza katika mtaa wa Waiyaki Real Gardens jijini Nairobi ambapo waAsia wengi walikuwa wakikaa.

Karanja Kibicho,Katibu wa Mambo ya Ndani.

Maafisa wa uhamiaji wamekagua stakabadhi za wageni hao, wanaoaminika walikuwa njiani kutoka Pakistan kuenda Saudia Arabia.

Video zinazosambaa mitandaoni zinaonyesha maafisa wa uhamiaji wakithibitisha hati za usafiri za raia hao wa kigeni.

https://twitter.com/i/status/1443492102562779136

Katibu mkuu wa Mambo ya Ndani, Karanja kibicho alizungumzia suala hilo akisema kuwa wageni hao wametokea Pakistan wakielekea Saudia Arabia na amekiri kuwa katika kipindi cha miezi minne, Kenya imeshuhudia ongezeko la waAsia wanaoingia nchini.

Katibu mkuu, amesema serikali itachukua hatua madhubuti kupunguza idadi ya wageni wanaopitia nchini kuelekea mataifa mengine.