Kwa kile ambacho kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga ameendelea kukitaja kama kuandaa maandamano kuipa serikali ya Rais Ruto shinikizo,Waziri wa usalama wa ndani nchini kenya Kithure kindiki amemuonya odinga dhidi ya maandamano.
“Wanaweza fanya mikutano ya umma na pia wanaweza andamana bila kuhitilifiana na biashara za wananchi wala kuwachochea watu kuzua vurugu,wanauhuru wa kuendesha siasa yao,sina shida na hilo”.
Kulingana na kindiki,kila mmoja anauhuru wa kuandamana ila iwapo maandamano haya yataingia doa na kuzua rabsha basi watalazimika kutumia maafisa wa polisi.
“Siku ambayo watavunja sheria kwa kukosesha wananchi amani,hiyo ndio siku ambayo watakumbana na mjeledi wa serikali kwa kutumia maafisa wetu wa polisi”.
Jumapili kiongozi wa upinzani nchini kenya Raila Odinga alitangaza kuandaa maandamano ya amani dhidi ya serikali ya rais william Ruto.
“Hakuna kitu ambacho atatufanyia sisi,aulize enzi za utawala wa nyayo chini ya rais mstaafu hayati Daniel Moi,hawezi kututishia eti anatukamata na kutupeleka mahakamani ,nyayo alijaribu hiyo na tukamwimbia wimbo wa sitarudi nyuma”
Muungano pinzani nchini kenya Azimio unatarajiwa kuandaa msururu wa mikutano ya hadhara kote nchini ambayo kilele chake kitatamatikia kaunti ya jijini Nairobi.