Majasusi wanasema kuwa mwanamke wa miaka 20 aliuawa na wengine watatu kujeruhiwa katika shambulio la bomu katika mgahawa maarufu kwa nyama ya nguruwe kaskazini mwa Uganda siku ya Jumamosi jioni.
Shambulio la bomu kwenye basi Jumatau lilitokea saa kadhaa baada ya kundi la Islamic State (IS) kudai kuhusika na shambulio jingine la bomu katika eneo ka Komamboga, kaskazini mwa mji mkuu wa Kampala, polisi walitaja shambulio hilo kuwa la kigaidi.
Shambulio la Jumatatu lilitokea siku tatu baada ya mlipuko mwingine Komambogo. “Eneo eneo limezingirwa kusubiri tathmini kamili,tutakuwa tunatoa maelezo kuhusu tukio hilo mara kwa mara,”msemaji wa polisi Fred Enanga amesema kwenye taarifa.
Walakini katika ujumbe kundi la wanamgambo kutoka Islamic State lilisema kuwa shambulio la bomu liliwauawa wawili na kujeruhi watano.
Oktoba 8, IS ilidai shambulio lake la kwanza Uganda katika kituo cha polisi mjini Kampala.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Greater Bushenyi, Bosco Otim, ni kati ya wale waliojeruhiwa kwenye shambulio la bomu kwenye basi katika barabara ya Kampala- Ishaka siku ya Jumatatu.