Mrembo atakae wakilisha Kenya katika shindano la Miss Universe Kenya asakwa,pengine ni wewe!

Miss Universe Kenya 2017 , Esther Mary Were

Miss Universe ni shindano la kimataifa la urembo linalofanyika kila mwaka na kuandaliwa na Miss Universe Organisation.

Lengo la kufanyika kwa shindano hilo ni kuweka wazi “masuala ya kibinadamu na ni sauti ya kuleta mabadiliko chanya ulimwenguni”.

Mshikilizi wa shindano hilo kwa sasa ni Andrea Meza kutoka Mexico, aliyetawazwa Mei 16 2021 mjini Hollywood Amerika.

Andrea Meza, Miss Universe 2021

Tangu shindano hilo lilipozinduliwa mwaka wa 1952, mataifa manne ya Afrika yameshinda tuzo hiyo, ikiwa ni mataifa ya Afrika Kusini, Namibia, Angola na Botswana.

Kenya ilifaulu kufika fainali ya mashindano hayo mwaka wa 2017 ilipowakilishwa na Mary Esther Were.

Mwaka wa 2019, Stacey Michuki aliiwakilisha Kenya katika mashindano ya 68 ya Miss Universe mjini Atlanta Georgia, Amerika.

Mashindano ya 70 ya Miss Universe 2021 yatafanyika mjini Eilat, Israel na Kenya itakuwa inawakilishwa katika mashindano hayo.

Ili kushiriki katika mashindano hayo, wasichana wanahitajika kuwa na umri wa miaka 18- 26, wasiwe wajawazito na watakaoshinda wasiwe wajawazito katika kipindi chote cha kushikilia wadhfa huo.

Wawakilishi wa Miss Universe pia, wanastahili kuwa na shahada ya chuo kikuu au wawe wanafanya kazi.

Kufikia mwaka wa 2012, wanaume waliobadili jinsia na kuwa wanawake waliruhusiwa kushirikriki katika shindano hilo, miaka sita baadae Angela Ponce wa Uhispania alishiriki katika shindano hilo akiwa mwanamume wa kwanza aliyebadili jinsia na kuwa mwanamke.

Taji la kwanza kuvaliwa na mshindi wa Miss Universe mwaka wa 1952, lilikuwa la familia ya kifalme ya Urusi, na lilivaliwa na mshindi wa kwanza wa shindano la Miss Universe kutoka Finland Armi Kuusela.

Armi Kuusela, Mshindi wa kwanza Miss Universe 1952

Taji la Miss Universe lina thamani ya $250,000 na huvaliwa na mshindi kwa sherehe rasmi na kurudishwa kwa shirikisho baada ya mwaka mmoja

Shindano la Miss Universe Kenya mwaka huu liko chini ya usimamizi mpya. Kituo cha habari na utangazaji cha Mwanzo TV Kenya kimeshinda leseni ya kuandaa mashindano hayo yatakayoanza Oktoba 30.

Ili ujisajili katika shindano hilo, unahitajika kuwa mwanamke mwenye umri wa miaka 18-27, Kuwa raia wa Kenya, Usiwe kwenye ndoa au kuwa na watoto, usiwe mjamzito wakati wa shindano hilo, uweze kuzumgumza kiingereza, uwe na pasipoti ya Kenya na uwe unasoma au kufanya kazi.

Kwa maelezo zaidi fuata link hii https://t.co/8ywjm9Lhwv?amp=1

Mshindi wa Miss Universe 2021, Andrea Meza.