Shule zafunguliwa nchini Kenya kwa Muhula wa Pili

Photo courtesy

Wazazi nchini Kenya wana wasiwasi juu ya hali ya usalama ya miundombinu ya mazingira ya shule, shule zinapofunguliwa kwa Muhula wa pili, Jumatatu, Mei 13, 2024, baada ya kuhairishwa mara mbili mfululizo na serikali kutokana na mvua ya mafuriko inayoendelea kushuhudiwa nchini humo.

Hata hivyo serikali ya Kenya kupitia wizara ya uchukuzi na usalama, imetuma maafisa wake katika maeneo yaliyoadhirika na mafuriko ili kuhakikisha usalama wa wanafunzi unadhibitiwa barabarani na shuleni.

Taarifa kutoka wizara ya elimu, imesema kuwa asilimia 95 ya shule ziko tayari kuanza tena muhula wa pili, huku hali katika baadhi ya taasisi za masomo katika kaunti saba zikiwa bado zinachunguzwa ili kuhakikisha unaafikia mazingira hitajika ya wanafunzi kutumia.

Kwa upande wa miundombinu za shule, wizara ya Elimu imesema kuwa wizara hiyo inashirikiana na taasisi nyingine za serikali, ili kirekebisha majengo yaliyoharibika katika baadhi ya shule, kabla ya kufunguliwa tena.