Search
Close this search box.
Africa

Siku ya kihistoria, Somalia inapoonesha filamu ya kwanza baada ya miaka 30

69

Somalia imeonyesha filamu yake ya kwanza baada ya miaka 30 chini ya ulinzi mkali Jumatano 22 nchi hiyo ikiwa na matumaini ya kukuza tamaduni zao.

Ukumbi huo wa sinema ulijengwa na wahandisi kutoka China mwaka 1967 kama zawadi kutoka kwa kiongozi wa China wakati huo Mao Zedong.Ukumbi huo umelengwa mara kadhaa na washambuliaji wa kujitoa mhanga na kutumiwa na wababe wa kivita kama maficho yao.

Jumatano 22 ilikuwa mara ya kwanza kwa filamu ya kisomali kuonyeshwa katika ukumbi huo.

“Huu utakuwa usiku wa historia kwa watu wa Somalia,inaonesha kuwa matumaini ya wengi yamefufuliwa baada ya miaka mingi ya changamoto”,mwelekezi wa ukumbi huo Abdikadir Abdi Yusuf alisema kabla filamu hiyo ilipoonyeshwa.

“kuonyeshwa kwa filamu hiyo kunawapa jukwaa wasanii, waigizaji, waandishi na waelekezi nafasi ya kuonyesha talanta zao.”

Filamu mbili “Hoos” na “Date from Hell” zilizoelekezwa na mwelekezi kutoka Somalia Ibrahim CM, zilionyeshwa.

Ibrahim CM,Mwelekezi wa filamu

Ingawaje, mji mkuu wa Mogadishu ulifahamika sana kwa kuonyesha filamu nyingi na kukuza tamaduni za nchi kwa kazi nyingi za usanii,yote hayo yaliisha baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilipozuka mwaka 1991.

Ukumbi huo ulijengwa upya baada ya mababe wa vita kuondoka na kufunguliwa rasmi 2012, wiki mbili baadae ulilipuliwa na kundi la Al-Shabab.

Baada ya miaka mingi ya ukumbi huo kufanyiwa ukarabati, mamlaka ya Mogadishu ilitangaza kuonyeshwa kwa filamu kwenye wiki hii. Kwa wasomali wengi, ilikuwa siku ya furaha na iliyojaa kumbukumbu ya siku zilizopita.

Comments are closed

Related Posts