KODI YA MAJENGO KWA NJIA YA UNUNUZI WA UMEME KUANZA Agosti 20,2021 TANZANIA
Serikali imesema inaanza utekelezaji wa kukusanya kodi ya majengo kwa mfumo mpya wa ukusanyaji kupitia ununuzi wa umeme. Zoezi hilo linaanza rasmi kesho Agosti 20,2021 na unafanyika chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Tanzania ukihusisha mita zote za umeme.