VUTE NIKUVUTE YAIBUKA KESI YA MBOWE
Shahidi wa sita kutoka upande wa Jamhuri SSP Sebastian Madembwe, ametoa ushahidi wake mbele ya Jaji Joachim Tiganga.
Shahidi wa sita kutoka upande wa Jamhuri SSP Sebastian Madembwe, ametoa ushahidi wake mbele ya Jaji Joachim Tiganga.
Mahakama Kuu, Divisheni ya makosa Rushwa na Uhujumu Uchumi imesomewa kielelezo cha kwanza cha ushahidi wa Jamhuri katika kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka ya ugaidi, inayomkabili kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania cha Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu.