MKUTANO WA SADC WAANZA LEO MALAWI
Mkutano wa 41 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi za SADC, umeanza leo #Malawi katika mji wa Lilongwe, ambapo unatarajia kumalizika kesho. Mkutano huo umehudhuriwa na wakuu wa nchi mbalimbali wa jumuiya hiyo huku Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassani akiwa ni miongoni mwao.