Jaji Siyani awataka Naibu Wasajili kutimiza majukumu yao kikamilifu
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mustapher Siyani amewataka Naibu Wasajili kutimiza majukumu yao kikamilifu ili kuchochea maendeleo ya Mahakama.
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mustapher Siyani amewataka Naibu Wasajili kutimiza majukumu yao kikamilifu ili kuchochea maendeleo ya Mahakama.
Shahidi wa kwanza upande wa utetezi Adam Kasekwa (Mshitakiwa wa 2), amepata kigugumizi cha kujibu maswali aliyokuwa akiulizwa na Wakili wa Serikali Abdallah Chavula. Hayo yamejiri leo katika Kesi Na.16/2021 inayowakabili Freeman Mbowe na wenzake 3, ambapo shahidi huyo ametoa ushahidi wake mbele Jaji Mustapha Siyani katika Mahakama Kuu Division ya Uhujumu Uchumi na Rushwa Ni baada ya Wakili wa Serikali Mwandamizi, Adballah Chavula, alipomuuliza mshtakiwa huyo mahakama ichukue kauli ipi kati ya maelezo yake aliyowahi kutoa mahakamani hapo, akidai alitoa maelezo yake ya onyo katika Kituo cha Polisi Mbweni mkoani Dar es Salaam, kwa mateso na maelezo aliyotoa akidai, alichukuliwa maelezo yake baada ya kutishwa na sio kuteswa.
Mvutano umeibuka katika geti la kuingia Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi nchini Tanzania baada ya baadhi ya viongozi wa CHADEMA, waandishi wa haabri na wanachama wa chama hicho kuzuiwa kuingia ndani ya chumba cha Mahakama.