Kigogo wa ZRB atumbuliwa kwa ufisadi wa bilioni 9.65, Zanzibar
Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi, ametengua uteuzi wa Kamisha Mkuu wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB), Salum Yussuf Ali na kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Usajili, Ukaguzi na Upelelezi wa Walipa Kodi wa mamlaka hiyo, Hashim Kombo Haji, ili kupisha uchunguzi wa upotevu wa shilingi bilioni 9.65.