Tanzania kuendelea kusimamia usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake kiuchumi
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mwanaidi Ali Khamis, mara baada ya kuwasili nchini akitikokea Ethiopia alikoshiriki Mkutano wa Sita wa Kamati Maalum ya Mawaziri ya Umoja wa Afrika wanaoshughulikia masuala ya Usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji Wanawake uliofanyika jijini Addis Ababa Ethiopia.