Nyimbo zilizomshambulia Rais Felix Tshisekedi zapigwa marufuku DR Congo
Maafisa wa udhibiti wa muziki Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) walikuwa wamepiga marufuku nyimbo mbili zinazomshambulia Rais Felix Tshisekedi. Kufikia Jumatano jioni maafisa wa udhibiti wa muziki walikuwa wameondoa marufuku kwa wimbo mmoja “Nini Tosali Te” (kwa lugha ya lingala, ‘’Ni kipi hatukufanya’)