Notice: Function _load_textdomain_just_in_time was called incorrectly. Translation loading for the wordpress-seo domain was triggered too early. This is usually an indicator for some code in the plugin or theme running too early. Translations should be loaded at the init action or later. Please see Debugging in WordPress for more information. (This message was added in version 6.7.0.) in /home/mwanzotv/public_html/wp-includes/functions.php on line 6114
Tahadhari ya UVIKO 19: Wapenzi nchini Thailand wahimizwa kuvaa barakoa wanaposhiriki kitendo cha ndoa katika siku ya Valentine - Mwanzo TV

Tahadhari ya UVIKO 19: Wapenzi nchini Thailand wahimizwa kuvaa barakoa wanaposhiriki kitendo cha ndoa katika siku ya Valentine

Huku wapenzi nchini Thailand wakijiandaa kuonyeshana mapenzi katika Siku hii ya Wapendanao, mamlaka ya afya inawataka wanandoa kushiriki ngona salama huku wakichukua tahadhari waepuke kuambukizana UVIKO 19 — ikiwa ni pamoja na kuvaa barakoa wakati wa kujamiana.

Idadi ya visa vya maambukizi ya kila siku vya UVIKO 19 katika nchi hiyo ambayo ni kitovu cha utalii katika eneo hilo la Kusini-mashariki mwa Asia imepanda kutoka takriban 8,000 mwanzoni mwa mwezi hadi karibu mara mbili katika wiki mbili zilizopita.

Mamlaka za afya zimeelezea wasiwasi kwamba tarehe 14 Februari inaweza kuzidisha hali hiyo, huku wakikubali watu wanashiriki kitendo cha ndoa katika siku zingine pia.

“UVIKO 19 sio ugonjwa wa zinaa, lakini mtu anaweza kuambukizwa ugonjwa huo kupitia kupumua kwa karibu na kubadilishana mate,”Mkurugenzi wa Ofisi ya Afya ya Uzazi Bunyarit Sukrat aliiambia AFP Ijumaa.

Alipendekeza wanandoa kufanya vipimo vya antijeni kabla kukutana ili kuzuia kupitisha virusi hivyo kwa wenzi wao.

Wapenzi wanahimizwa “kuepuka kushiriki ngono huku wakitazamana ana kwa ana na kubusiana sana,” na kuhakikisha  wanatumia kondomu na vidonge kuzuia mimba zisizopangiwa Bunyarit alisema.

Siku ya Valentine ni maarufu sana nchini humo na inachukuliwa kuwa siku bora  kwa wanandoa kufunga pingu za maisha.

Mara nyingi kuna foleni ndefu katika ofisi za usajili wa ndoa, hasa katika wilaya ya Bangkok ya Bang Rak, ambayo hutafsiriwa kuwa “wilaya ya mapenzi” katika lugha ya Thai.