Tajiri wa Misri ahukumiwa miaka 3 jela kwa kuwanyanyasa kijinsia watoto wadogo

Mahakama ya Misri imemhukumu mfanyabiashara mmoja kifungo cha miaka mitatu jela kwa ulanguzi na kuwalawiti wasichana saba wenye umri chini ya miaka 26 katika kituo cha watoto yatima alichoanzisha, duru za mahakama zilisema.

Tajiri huyo Mohamed el-Amin anayemiliki vyombo vya habari na majumba mengi Misri alikamatwa mwezi Januari kwa tuhuma kwamba aliwanyanyasa kingono wasichana wadogo katika kituo cha watoto yatima huko Beni Suef, yapata kilomita 100 (maili 60) kusini mwa Cairo.

Amin, ambaye alimiliki mtandao maarufu wa televisheni wa CBC kabla ya kuuzwa mwaka wa 2018, anakabiliwa na kifungo cha miaka 25 jela.

Amin anaweza kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo ya miaka mitatu jela, chanzo cha mahakama kiliiambia AFP.

Kesi hiyo iliwekwa wazi kwa umma baada ya ukurasa wa Facebook kumshutumu Amin kwa kuwanyanyasa kingono wasichana wadogo.

Mbali na mashahidi ambao “walithibitisha ushuhuda wa waathirwa:, picha zilipatikana kwenye simu ya mfanyabiashara  huyo wakati wa uchunguzi na rekodi zilitolewa za waathiriwa wakielezea shambulio hilo, vyanzo vya mahakama vilisema.

Upande wa mashtaka ulisema waathiriwa walimshutumu Amin kwa kuwanyanyasa mara kwa mara “bila idhini yao.”

“Alitumia madaraka yake vibaya dhidi ya wasichana yatima, ambao aliwanyanyasa kijinsia na kutishia kuwafukuza (kutoka kwenye kituo cha watoto yatima) ikiwa wangemripoti,”

Miaka mitatu ndiyo adhabu nyepesi zaidi iliyotolewa na sheria ya Misri, ambayo inaweka kifungo cha juu cha miaka 15 kwa unyanyasaji wa kijinsia.

Lakini kanuni ya adhabu inaweka kifungo cha chini cha miaka saba ikiwa mwathiriwa ni mtoto mdogo au kama mkosaji ana mamlaka juu ya mwathirika, na adhabu ya juu ya kifungo cha maisha jela (miaka 25) ikiwa masharti yote mawili yametimizwa.