Search
Close this search box.
Asia

Taliban inataka kushirikishwa katika mijadala ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) Marekani

319

Taliban imeagiza kupewa nafasi na kuhutubia viongozi wa mataifa tofauti duniani waliokongamana jijini Newyork Marekani kwa mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Kamati kuu ya Umoja wa mataifa imesema itafanya maamuzi ila huenda kundi hilo lisipate nafasi ya kuhutubia viongozi hao wakati mkutano ukiendelea.

Kundi la Taliban limemteua msemaji wao mwenye makazi yake mjini Doha Qatar, Suhail Shaheen, kama balozi wa Afghanistan kwa Umoja wa Mataifa.

Suhail Shaheen, Balozi wa Taliban UN

Kulingana na msemaji wa UN, ombi la Taliban kutaka kushirikishwa kwa majadiliano ya Umoja wa mataifa linajadiliwa na wanachama wa Umoja wa Mataifa kutoka Marekani,China na Urusi, ila kwa sasa,Ghulam Isaczai atasalia kuwa balozi wa Afghanistan kwa Umoja wa Mataifa na anatarajiwa kutoa hotuba yake katika siku ya mwisho ya kongamano hilo,Taliban kwa upande wao hawamtambui Ghulam Isaczai na wanasema kuwa hawakilishi Afghanistan.

Hadi sasa hakuna serikali yoyote ambayo imetambua Taliban kama serikali mpya ya Afghanistan na kwa umoja wa Mataifa kukubali mtu aliyependekezwa na Taliban kama  balozi wa UN itakuwa hatua muhimu katika kuikubali serikali hiyo mpya. Taliban imesema pia kuwa mataifa mengi hayamtambui rais wa zamani Ashraf Ghani kama kiongozi wa Afghanistan.

Mara ya mwisho Taliban walipokuwa uongozini kati ya 1996 na 2001, baada ya kupindua serikali ya wakati huo, balozi wa wakati huo aliendelea kuiwakilisha Afghanistan kwa Umoja wa Mataifa. Qatar, imewaomba viongozi kuendeleza mazungumzo na Taliban, wakisema kuwa kutenga Taliban kutaleta migawanyiko zaidi.

Qatar imekuwa chombo muhimu katika kukuza mawasiliano kati ya Taliban na Marekani yaliyochangia makubaliano ya kuondoka kwa majeshi ya Marekani nchini humo.

Comments are closed

Related Posts