Tuzo za BET, ambazo huwatunuku watumbuizaji weusi katika muziki, uigizaji, utamaduni, na michezo, zilitolewa Jumapili.
Mwigizaji Taraji P. Henson alikuwa mwenyeji katika tamasha hiyo, ambalo ilianza kwa wimbo kutoka kwa msanii Lizzo akiimba wimbo wake mpya, ‘About Damn Time.’
Waimbaji wa Nigeria Tems na Wizkid walikuwa miongoni mwa Waafrika walioshinda tuzo.
Baadhi ya waigizaji na waliopokea tuzo walitoa wito wa kuchukuliwa hatua baada ya uamuzi wa Mahakama ya Juu kubatilisha Roe v. Wade siku ya Ijumaa.
Msanii Brandy alifanya onyesho la kushtukiza na Jack Harlow, naye Mariah Carey akaimba kwa sauti yake nyororo akishirikiana na Latto.
Sean ‘Diddy’ Combs alipokea tuzo ya Lifetime Achievement.
Alisherehekewa na kundi la wasanii wenzake na washiriki wa zamani kama Mary J. Blige na Kanye West.
Will Smith, ambaye alizua utata kwenye Tuzo za Academy kwa kumpiga kofi Chris Rock jukwaani muda mfupi kabla ya kushinda tuzo ya mwigizaji bora katika tuzo za Oscar, alishinda Tuzo ya BET ya mwigizaji bora siku ya Jumapili.
Orodha kamili ya walioshinda tuzo katika vitengo tofauti ni:
Best Female R&B/Pop Artist
Jazmine Sullivan
Best male R&B/Pop Artist
The Weeknd
Best Group
Silk Sonic (Bruno Mars and Anderson .Paak)
Best Collaboration
Wizkid feat. Justin Bieber & Tems – “Essence”
Best Female Hip Hop Artist
Megan Thee Stallion
Best Male Hip Hop Artist
Kendrick Lamar
Video of the Year
Silk Sonic (Bruno Mars & Anderson .Paak) – “Smokin Out The Window”
Video Director of the Year
Anderson .Paak a.k.a. Director .Paak
Best New Artist
Latto
Album of the Year
Silk Sonic (Bruno Mars & Anderson .Paak) – “An Evening with Silk Sonic”
Best International Act
Tems (Nigeria)
Best Movie
“King Richard”
Best Actor
Will Smith – “King Richard”
Best Actress
Zendaya – “Euphoria” / “Spider-Man: No Way Home”
Youngstars Award
Marsai Martin
Sportswoman of the Year Award
Naomi Osaka
Sportsman of the Year Award
Stephen Curry