Thomas Sankara kiongozi wa zamani wa Burkina FasoAlipewa jina la utani la Che Guevara wa Afrika, Thomas Sankara alikuwa na azma ya “kuondoa ukoloni” nchini Burkina Faso na katika bara zima.Lakini ndoto zake za mapinduzi zilikatizwa kikatili alipouawa kwa kupigwa risasi katika mapinduzi ya 1987 baada ya miaka minne tu madarakani.Siku ya Jumatano, mahakama ya kijeshi ilitoa mihula ya maisha kwa wanaume watatu wanaotuhumiwa kutekeleza majukumu muhimu katika mauaji yake, akiwemo aliyekuwa swahiba wake wa zamani, Blaise Compaore, ambaye alimrithi kama rais na kuendelea kutawala kwa miaka 27.Licha ya muda wake mfupi madarakani, Sankara anasalia kuwa mtu anayeheshimika.Wakati wa maandamano makubwa ambayo yalimuangusha Compaore mwaka wa 2014, vijana walibeba picha za Sankara juu juu — ingawa wengi walikuwa hawajazaliwa wakati wa utawala wa kiongozi huyo.“Sankara ni falsafa nzima, ni fikra , njia ya maisha. Sankara ni fahari ya Afrika,” mwalimu wa shule ya upili Serge Ouedraogo alisema.“Leo hii, tunaweza kusema kwamba Sankara anawakilisha dira kwa watu wa Burkina Faso. Yeye ni mwongozaji, ndiye aliyewasha njia ya matumaini kwa watu.”Kupanda madarakani –Alizaliwa mnamo Desemba 21, 1949 huko Yako kaskazini mwa Burkina Faso, Sankara alilelewa katika familia ya Kikristo, baba yake mkongwe alikuwa mwanajeshi.Alikuwa na umri wa miaka 12 tu wakati nchi hiyo ilipopata uhuru kutoka kwa Ufaransa.Baada ya kumaliza shule ya upili huko Ouagadougou, alipitia mafunzo ya kijeshi nje ya nchi.Alikuwa Madagaska kwa ajili ya uasi wa 1972 ambao ulimpindua Rais Philibert Tsiranana, aliyezingatiwa na maadui kuwa mtawala wa ukoloni wa zamani wa Ufaransa.Aliporudi katika nchi yake mwaka wa 1973, Sankara alipewa jukumu la kuwapa mafunzo ya kijeshi vijana, na alijitokeza wakati na kupigana katika vita vya mpaka na Mali mwaka 1974-1975Baada ya mapinduzi ya mwaka 1980, kiongozi mpya, Kanali Saye Zerbo, alimteua Sankara kuwa katibu wake wa mambo ya nje wa habari.Lakini maoni yake makali yalimfanya ajiuzulu mwaka mmoja na nusu baadaye.Sankara aliteuliwa kuwa waziri mkuu mnamo Januari 1983 baada ya mapinduzi mengine ya kijeshi, ambayo yalisababisha mzozo wa madaraka kwenye jeshi.Alikamatwa Mei 1983 lakini akafanywa rais mwezi Agosti baada ya mapinduzi mengine — haya yaliyoongozwa na rafiki yake wa karibu Compaore.Akiwa na umri wa miaka 33 tu, Sankara aliwakilisha vijana wa Kiafrika kwa uadilifu.Alibadilisha jina la nchi hiyo kutoka enzi ya ukoloni ya Upper Volta hadi Burkina Faso – “nchi ya watu waaminifu.”Alihamia katika ikulu ya rais na mkewe na wanawe wawili, pamoja na gitaa lake — alikuwa mchezaji mzuri, kulingana na watu wa wakati wake.Pia alileta magari aina ya Renault 5 yaliyokuwa mitumba na akaweka gari hilo dogo kama gari la wafanyikazi wote wa serikali, akiondoa magari makubwa. Kukemea vita vya ‘mabeberu’Mwembamba na mkakamavu, Sankara kila mara alipenda kuvalia sare ya jeshi, na kwenye mkanda wake alipenda kuonyesha bastola yenye aliyopewa na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Il-Sung.Vipaumbele katika mpango wake wa mageuzi ilikuwa ni pamoja na kupunguza idadi ya watumishi wa umma, kuboresha huduma za afya, kusoma na kuandika, kujitosheleza kwa chakula, hatua za kuwasaidia wakulima wadogo, kampeni za chanjo na kujenga maduka ya dawa vijijini.Alipiga marufuku ukeketaji na ndoa za kulazimishwa, miongoni mwa hatua nyingine za kukuza haki za wanawake, ambazo alizisimamia yeye mwenyewe.“Lazima tuondoe ukoloni akilini mwetu,” alitangaza.Hata hivyo alianza kukandamiza vyama vya wafanyakazi na upinzani wa kisiasa, na kuvunja mgomo wa walimu kwa kuwafuta kazi.Sankara pia aliitaka Afrika kukataa kulipa deni lake kwa nchi za Magharibi na alizungumza katika Umoja wa Mataifa kukemea vita vya ‘kibeberu,’ ubaguzi wa rangi na umaskini.Pia alitetea haki ya Wapalestina ya kujitawala.Uhusiano wa Burkina Faso na Ufaransa na nchi kadhaa jirani, ikiwa ni pamoja na Ivory Coast ya Felix Houphouet Boigny na Togo ya Gnassingbe Eyadema, ulizidi kuwa mbaya.Wakati huohuo alichukuliwa kuwa mwandani wa karibu sana na kiongozi wa Libya Moamer Kadhafi na kiongozi wa Ghana ya Jerry Rawlings na baadhi ya nchi za Magharibi.Sankara hata alimpa Francois Mitterrand somo katika haki za binadamu mwaka 1986 baada ya rais wa Ufaransa kumpokea Pieter Botha, kiongozi wa utawala wa kibaguzi wa Afrika Kusini, mjini Paris.“Anaenda mbali zaidi kuliko inavyohitajika kwa maoni yangu,” Mitterrand, Msoshalisti, alitoa maoni yake kwa huzuni.Mnamo Oktoba 15, 1987, baada ya kuitwa kwenye kikao kisicho cha kawaida cha baraza la mawaziri, Sankara alishambuliwa na wanajeshi wenzake wakati wa mapigano yaliyomweka Compaore madarakani.Alikuwa na umri wa miaka 37 tu.