Search
Close this search box.
Sports
Khalifa International Stadium on November 18, 2022

Utafiti wa hivi punde umeonyesha kuwa mashabiki wa soka wanaohudhuria mechi za kombe la Dunia nchini Qatar watatoa karibia asilimia 40 zaidi kununua tiketi za mechi ikilinganishwa na wale waliotazama toleo la mwaka wa 2018 nchini Urusi huku tikiti za fainali zikigharimu pauni 684 (Ksh. 99,100).

Wakati mashabiki nchini Urusi walilipa takriban pauni 214 (31, 1000) kwa tikiti za mechi nchini Qatar zinagharimu pauni 286 (41,000) kulingana na utafiti wa Keller Sports.

Bei za tikiti nchini Qatar ni ghali zaidi kuwahi kuuzwa katika historia ya michezo ya Kombe la Dunia katika kipindi cha miaka 20 iliyopita, huku zile za fainali zikiwa juu kwa asilimia 59 kuliko miaka iliyopita.

“Kombe la Dunia nchini Qatar tayari linachukuliwa kuwa Kombe la Dunia ghali zaidi kuwahi kushuhudiwa. Ujenzi wa viwanja sita vipya na ukarabati kamili wa viwanja vingine viwili nchini unasemekana kugharimu karibu dola bilioni 3,” Utafiti huo ulisema.

“Pesa nyingi zaidi zilitumika katika kupanua miundombinu ya mji mkuu wa Doha, kama vile njia za usafiri na ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa.”

“Haishangazi kwamba Kombe la Dunia nchini Qatar pia ni Kombe la Dunia lenye tikiti za bei ghali zaidi kwa wastani.”

Awali FIFA ilisema karibu tiketi milioni tatu katika viwanja vinane vya Qatar zimeuzwa kabla ya kindumbwedumbwe chenyewe cha Novemba 20-Disemba 18  ambalo ni la kwanza Mashariki ya Kati.

Tiketi za Kombe la mwaka 2006 nchini Ujerumani zilionekana kuwa za bei nafuu zaidi katika miaka 20 iliyopita, kwani iligharimu  takriban pauni 100 kwa mechi wakati tiketi za fainali za Olympiastadion ya Berlin ziligharimu pauni 221 (Ksh 32,000) kwa kiti.

Comments are closed