“Tumechukua uongozi wa nchi kukomesha ufisadi na umaskini “ Kanali Mamady Doumbouya

MAPINDUZI GUINEA

Jumapili 5 Septemba, Kanali wa Vikosi Maalum katika serikali ya Guinea Mamady Doumbouya na jeshi lake wamempindua Rais Alpha Conde.Katika taarifa ya Mamady kupitia chombo cha habari cha kitaifa, amesema umaskini, ufisadi na rushwa uliokithiri nchini humo umechangia katika mapinduzi hayo, akiongeza kuwa katika siku za hivi karibuni bei ya mafuta ilikuwa imepanda kwa 20%.

Wanajeshi wamefunga mipaka ya nchi kavu na ya anga baada ya kufanya mapinduzi na kutangaza kuivunja katiba ya nchi, na kuwataka mawaziri waliohudumu chini ya Rais Alpha Conde kuhudhuria mkutano Jumatatu 6 Septemba, na yeyote atakeyekosa kuhudhuria mkutano huo atachukuliwa kama muasi.

Wanajeshi wametangaza kuwa nchi hiyo itakuwa chini ya serikali ya mpito na kuweka katika marufuku ya kutotoka nje kwa muda usiojulikana.

Mapinduzi hayo yamelaaniwa na Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika, huku Rais wa taifa jirani la Liberia George Weah, akiitisha kuachiliwa mara moja kwa Rais Alpha Conde.Rais Weah amelitaka jeshi hilo kuzingatia kanuni za utawala wa raia na demokrasia.