Search
Close this search box.
Africa

Tunisia yaidhinisha katiba mpya baada ya watu wachache kujitokeza kupiga kura

13
Rais wa Mamlaka Huru ya Juu ya Uchaguzi, Farouk Bouasker, akzungumza na waandishi wa habari kuhusu matokeo ya mwisho ya kura ya maoni kuhusu rasimu ya katiba iliyotolewa na Rais wa nchi hiyo, mjini Tunis Julai. 26, 2022. (Photo by Anis MILI / AFP)

Tunisia imeidhinisha katiba mpya inayotoa mamlaka makuu kwa ofisi ya Rais Kais Saied, bodi ya uchaguzi ilisema, baada ya kura ya maoni iliyokuwa na wapiga kura wachache kuunga mkono katiba hiyo mpya.

Wapinzani wa Saied walishutumu bodi ya uchaguzi inayodhibitiwa na Saied kwa udanganyifu na kusema kura yake ya maoni, iliyofanyika Jumatatu, haikufaulu.

Siku ya Jumanne jioni, mkuu wa tume ya uchaguzi Farouk Bouasker aliwaambia waandishi wa habari kuwa mamlaka hiyo “inatangaza kukubaliwa kwa rasimu ya katiba mpya ya Jamhuri ya Tunisia.” kwa kuzingatia matokeo ya awali, kwa asilimia 94.6 ya kura za kuunga mkono kuwepo kwa katiba mpya halali, kwa asilimia 30.5 ya watu waliojitokeza.

Kura ya Jumatatu ilijiri mwaka mmoja baada ya rais kuifuta serikali na kusimamisha bunge katika pigo kubwa kwa demokrasia pekee iliyoibuka kutokana na ghasia za Arab Spring za 2011.

Kwa baadhi ya wananchi wa Tunisia, hatua zake zilizua hofu ya kurejea kwenye utawala wa kiimla, lakini walikaribishwa na wengine, waliochoshwa na mfumuko mkubwa wa bei na ukosefu wa ajira, ufisadi wa kisiasa na mfumo ambao walihisi umeleta maboresho machache.

Kulikuwa na mashaka kidogo kwamba kampeni ya kuunga mkono katiba mpya ingeshinda, utabiri ulioonyeshwa katika kura ya maoni iliyofanywa na kikundi huru cha Sigma Conseil.

Wapinzani wengi wa Saied walitoa wito wa kususia, na ingawa waliojitokeza walikuwa wachache, walikuwa wengi kuliko idadi iliyotarajiwa.

“Tunisia imeingia katika awamu mpya,” Saied aliwaambia wafuasi wake waliokuwa wakisherehekea baada ya upigaji kura kufungwa.

“Walichokifanya watu wa Tunisia… ni somo kwa ulimwengu, na somo kwa historia kwa kiwango ambacho mafunzo ya historia yatapimwa,” alisema.

Lakini Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilisema Jumanne ilibainisha “wasiwasi wake kwamba katiba mpya inajumuisha vipengee ambavyo vinaweza kuathiri ulinzi wa haki za binadamu na uhuru wa kimsingi.”

Na muungano wa upinzani wa National Salvation Front nchini Tunisia ulishutumu bodi ya uchaguzi kwa kughushi takwimu za waliojitokeza kupiga kura.

Mkuu wa NSF Ahmed Nejib Chebbi alisema takwimu “ziliongezwa na haziendani na kile waangalizi waliona siku ya kupiga kura.

Bodi ya uchaguzi ‘si ya kuaminika na takwimu zake si za kweli,” alisema.

Saied, profesa wa sheria mwenye umri wa miaka 64, alivunja bunge na kutwaa udhibiti wa mahakama na tume ya uchaguzi Julai 25 mwaka jana.

Wapinzani wake wanasema hatua hizo zililenga kuweka utawala wa kiimla zaidi ya muongo mmoja baada ya kuanguka kwa dikteta Zine El Abidine Ben Ali, lakini wafuasi wake wanasema ni muhimu baada ya miaka mingi ya ufisadi na machafuko ya kisiasa.

“Baada ya miaka 10 ya kukatishwa tamaa na kushindwa kabisa katika usimamizi wa serikali na uchumi, watu wa Tunisia walitaka kuondokana na mambo ya zamani na kuchukua hatua mpya — bila kujali matokeo,” alisema Noureddine al-Rezgui, mwanasheria.

Utafiti wa wapiga kura waliounga mkono katiba mpya iliofanywa na runinga ya serikali ilipendekeza “kurekebisha nchi na kuboresha hali ilivyo nchini”.

Asilimia kumi na tatu walitsema “washawishiwa na katiba mpya.”

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yameonya kuwa rasimu hiyo inatoa mamlaka makubwa, ambayo hayathibiti kwa urais, inamruhusu Saied kuteua serikali bila idhini ya bunge na kumfanya kuwa vigumu kabisa kumwondoa madarakani.

Comments are closed

Related Posts