Hatua ya mahakama ya upeo nchini Kenya kuamua kwamba wapenzi wa jinsi moja (LGBTQ) nchini humo wanauhuru wa kujumuika pamoja na kuunda kundi linalotambulika kisheria imezidi kuzua hisia mseto.
Viongozi wa kidini na wale wa kisiasa serikalini wamejitokeza kushtumu uamuzi huo wa mahakama ambao wameutaja kama kinyume na mila na desturi.
Viongozi wa dini ya kikiristu kutokaka makanisa tofauti yakiwemo ya SDA na CITAM wamedai kuwa wamesikitishwa na uamuzi huo ambao wamutaja kama wenye udanganyifu mwingi unaopotosha jamii nchini Kenya.
Kanisa la Kiadventista, SDA Kupitia askofu Vincent Oyugi wa tawi la Homa bay sasa limelitaka bunge la kitaifa kuunga mkono mswada unatarajiwa kuwasilishwa bungeni na mbunge wa Homabay Peter Kaluma akishinikiza kuharamishwa kwa shughli zinazohusiana na wapenzi wa jinsia Moja (LGBTQ) nchini Kenya.
“Tunakashifu vikali,haikubaliwi katika bibilia na chukizo kubwa kwa mwenyezi Mungu.Waumini wa wakrito wanafaa kukataa jambo hili la wapenzi wa jinsia moja LGBTQ maana litachangia kuendeleza usherati nchini Kenya,” alisema askofu Vincent Oyugi
Upande mwingine Kanisa la CITAM nalo kupitia barua iliyotiwa wino na Askofu Calisto Odede wameelezea maskitiko yao kuhusu uamuzi huo.
“Tusikitishwa zaidi na uamuzi huu,hii inamaanisha kuwa wanaovunja sheria wengine wakiwemo walawiti na wanaojihusisha katika mapenzi na watu wenye ukoo wao wanafaa pia kuhalalishwa na kuruhusiwa kujumuika pamoja”
Tayari mwanasheria mkuu nchini Kenya Justin Muturi ameapa kuelekea mahakamani kupinga uamuzi huu wa mahakama ya upeo nchini Kenya.
Hisia sawa zimetolewa na spika wa bunge la kitaifa nchini Kenya Moses Masika Wetangula ambaye amekashifu mahakama akisema kuwa wanajukumu la kudumisha tabia na desturi ya wakenya.
Kulingana na Wetangula,taifa la Kenya limejikita katika dini ambayo hairuhusu wapenzi wa jinsia Moja.
Uamuzi huo sasa unawapa wapenzi wa jinsia moja uwezo wa kutafuta kutambuliwa rasmi na Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.