Misururu zaidi ya michezo ya ndondi yamepangwa kote nchini Kenya kama sehemu moja ya kukuza umaarufu na ushirikishaji wa jamii katika fani hio.
Kampuni ya mchezo wa Kamari, BetNare, inasema imejitolea kufanya kazi kwa karibu na shiriko la ndondi nchini kenya na wakuzaji wa mchezo huo kwa minajili ya kukuza mchezo wa masumbwi mashinani
Uamuzi huu umefuatia matukio mawili ya ndondi ya kufana yaliyofana kwa muda wa miezi miwili iliyopita katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa KICC mnamo Januari na wa hivi majuzi katika ukumbi wa Kasarani.
“Tunashauriana na waandalizi wa ndondi ya kimataifa na wakuzaji wa mchezo huo kuona jinsi tunavyoweza kufanya kazi pamoja ili kuwa na spoti ya ndondi katika maeneo mengine ya nchi,” ilisema kampuni ya BetNare.
“Tumekuwa na ndondi mawili yenye mafanikio makubwa sana jijini Nairobi na ni wazi kwamba basi michezo inapendwa na watu wengi na inazidi Kukua. Sasa tunatakiwa kupeleka matukio mengi zaidi maeneo mengine ya nchi, pia nafurahisha kusikia kwamba Bi Nancy Matimu (mkurugenzi mkuu wa Multichoice) anapania kuendeleza michezo huu kwa ujumla’’
“Kampuni ya BetNare imejitolea kusaidia kujenga upya mchezo huo ambao wakati mmoja ulikuwa maarufu sana. Tunataka kusaidia kuibua vipaji vipya na kuwa na mastaa kama Robert Wangila Napunyi…
Mwishoni mwa juma, mapigano kadhaa ya ndondi yalifanyika katika Ukumbi Kasarani
Mtanzania Karim “Mtu Kazi” Mandonga alimbwaga Mganda Kenneth Lukyamuzi wa Uganda katika uamuzi wa mgawanyiko wa majaji na kutwaa taji la PST.
Kwingineko mkenya Daniel Wanyonyi alimshinda mpinzani wa Uganda Charles Kakande katika raundi sita.