Ugonjwa wa monkeypox walipuka upya DR Congo


Serikali ya Maniema, jimbo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), imetangaza rasmi Alhamisi kulipuka kwa ugonjwa wa monkeypox.

Visa 191 vya ugonjwa wa monkeypox vimeripotiwa ikiwemo  vifo 24 vilivyoripotiwa tangu mwezi Septemba 27, 2021, Afani Idrissa Mangala, kaimu gavana wa Maniema, ametangaza kwenye taarifa kuhusu mlipuko huo.

Mlipuko huo ulithibitishwa baada ya uthibitisho wa sampuli zilizotumwa kwa Taasisi ya Kitaifa ya Utafiti wa Tiba (INRB), alisema Mangala, akitoa wito kwa watu kuwa waangalifu na kushauriana na vituo vya afya iwapo watapat dalili zozote za ugonjwa huo ikiwemo homa kali.

Mnamo Novemba 2021, mlipuko wa surua ulizuka katika mkoa huo huo.

Visa vya kwanza vya ugonjwa wa monkeypox viligunduliwa mwaka 1970 nchini DRC. Homa, kuwasha vidole vya miguu, kuumwa na kichwa, maumivu ya misuli, na uvimbe wa nodi za limfu, miongoni mwa mambo mengine, zimetambuliwa kuwa dalili za ugonjwa huo.

Ugonjwa huo sio hatari na unaweza kutibiwa kwa kupata chanjo ya ndui.